Aliye Choma Moto Basi La Sai Baba Ahukumiwa
Aliye Choma Moto Basi La Sai Baba Ahukumiwa
Mahakama Wilayani Korogwe mkoani Tanga, imewahukumu washtakiwa Sita kifungo cha miaka Mitatu Jela au kulipa Faini ya kiasi cha Shilingi Milioni 1 kwa kila mshtakiwa kwa kosa Kuharibu Mali ya Kampuni ya SaiBaba kinyume na Sheria
Waliokutwa na hatia ya Kutenda kosa hilo ni pamoja na Bashiru Abdallah Shehoza (25), Bakari Amosi Anania (24), Bakari Ally Muhando (29), Ramadhani Haruna Malaba (24), Benjamin William Shehoza (25) na Abdallah Omary Koko (25) wote wakiwa ni wakazi wa Wilaya ya Korogwe
Imeelezwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi wa Korogwe Mhe. Fransisca Maguiza, Washtakiwa hao sita walitenda kosa kuchoma moto basi la Kampuni ya Sai Baba, iliyokuwa Ikitokea Jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Arusha, mnaml tarehe 17/2/2024 katika eneo la Shamba darasa, katika kijiji cha Msamnbiazi, kata ya Mtonga
Hata Hivyo hakimu Fransisca MaguiÄ°za amesema washtakiwa hao wana nafasi ya kukata Rufaa ndani ya siku 30 au kuendelea kutumikia adhabu ya miaka mitatu au Faini ya Milioni 1 ambapo Kesi hiyo iliendeshwa na wakili wa Serikali Bi. Sarah Wangwe