Amuuwa Baba Akidai Anaharibu Mimba
Amuuwa Baba Akidai Anaharibu Mimba
Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linamshikilia Juhudi Mkosa (30), Mkazi wa Kijiji cha Kijombe, Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe kwa tuhuma za kumuua Baba yake baada ya kumtuhumu kujihusisha na ushirikina uliodaiwa kusababisha mimba za Mke wake kuharibika mara kwa mara.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamouda Banga amesema Mtuhumiwa anadaiwa kutenda tukio hilo Novemba 29, 2025 kwa kumuua Baba yake, Ernesto Mkosa kutokana na imani kwamba alikuwa akihusika na vitendo vya ushirikina.
Kamanda Banga amesema katika mahojiano na Vyombo vya upelelezi, Mtuhumiwa alikiri kutenda tukio hilo na kueleza kuwa alichukua hatua hiyo kutokana na imani yake kuwa Baba yake ndiye aliyekuwa chanzo cha changamoto za ujauzito wa Mke wake.
“Sababu halisi iliyopelekea Mtuhumiwa huyu kutenda mauaji hayo ni kumtuhumu Mzazi wake ushirikina na kudai kwamba Mke wake alikuwa akipata changamoto ya mimba kuharibika mara kwa mara,” amesema Kamanda Banga.
Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, huku Mtuhumiwa akitarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika





