Jela Maisha Kwa Kumlawiti Mtoto wa Miaka 11
Jela Maisha Kwa Kumlawiti Mtoto wa Miaka 11
Mahakama ya Mkoa wa Tanga imemhukumu Said Yunusu maarufu kama Big Sela (20), kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti Mtoto mwenye umri wa miaka 11.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mwanaheri amesema Mahakama imeridhishwa na ushahidi uliowasilishwa na Upande wa Mashtaka ambao umethibitisha shtaka dhidi ya Mshtakiwa.
Kwa mujibu wa maelezo ya kesi hiyo yenye Namba CC No. 2829/2026, Mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho ni Mwanafunzi wa Darasa la Nne.
Mahakama imesema hukumu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Sheria, huku Said Yunusu akitakiwa kutumikia kifungo cha maisha jela.





