Anaye Daiwa Kuendesha Pesa Ya Upatu Ajifungua Gerezani.

Anaye Daiwa Kuendesha Pesa Ya Upatu Ajifungua Gerezani.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeelezwa kuwa Mkurugenzi wa kampuni ya mikopo ya Atlantic Micro Credit Limited, Wendy lshengoma (38) anayekabiliwa na mashitaka ya kuendesha biashara ya upatu, ameshindwa kufika mahakamani hapo kutokana na kujifungua.

Mshtakiwa huyo ambaye alifutiwa shitaka moja la kutakatisha fedha, amejifungua mtoto wa kiume, ljumaa Februari 21, 2025 akiwa gerezani.

Ishengoma na wenzake watatu wanakabiliwa na mashitaka ya kuongoza gernge la uhalifu, kuendesha biashara ya upatu na kutakatisha Sh3.6 bilioni.

Wakili wa Serikali, Frank Rimoy ametoa taarifa hiyo leo Jumanne Februari 25, 2025 wakati kesi hiyo ya uhujumu uchumi 30853/2024 ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Rimoy ametoa taarifa hiyo mbele ya hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya, ambapo amedai ndugu wa mshtakiwa pamoja na taarifa aliyopewa kutoka magereza, inaeleza Wendy amejifungua mtoto wa kiume wiki iliyopita, hivyo ameshindwa kufika mahakamani hapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button