Heche: Tanzania Ni Tajiri Lakini Wananchi Wake Wanateseka Kwa Umaskini
Heche: Tanzania Ni Tajiri Lakini Wananchi Wake Wanateseka Kwa Umaskini
Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche, amesema licha ya Tanzania kuwa na utajiri mkubwa wa rasilimali, chama tawala (Chama Cha Mapinduzi-CCM) kimeshindwa kuzitumia kwa ufanisi kuboresha maisha ya wananchi.
Akizungumza leo, Jumatano Februari 12, 2025, mkoani Simiyu katika hafla fupi ya mapokezi yake akielekea mkoani Mara baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo
Januari 22. Heche amesema hali ya maisha ya Watanzania bado ni duni.
“Baada ya miaka 63 ya uhuru, hakuna mabadiliko makubwa. Chakula ni tatizo, maji ni shida na mwanamke akijifungua hata mume wake anaingia kwenye msongo
wa mawazo,’ amesema Heche.
Ameongeza kuwa Tanzania ina utajiri mkubwa wa dhahabu kutoka Tarime hadi Singida, Mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama na maziwa makubwa, lakini bado
wananchi wanakabiliwa na umaskini wa kupindukia.
“Tunapaswa kuwa nchi inayotoa misaada kwa mataifa mengine, lakini leo watu wetu wanashindwa hata kupata chakula,” ameongeza Heche. Pia, amewakosoa viongozi wa sasa, akisema mawazZO yao yamechoka na wanarudia wale wale waliokuwepo tangu uhuru.