Aliyekuwa Gavana Kenya Ahukumiwa Miaka 12 Jela Mkewe Apigwa Faini
Aliyekuwa Gavana Kenya Ahukumiwa Miaka 12 Jela Mkewe Apigwa Faini
Aliyekuwa Gavana wa Jimbo la Kiambu, Ferdinand Waititu amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela ama kulipa faini ya kiasi cha Sh1.08 bilioni (Ksh53.8 milioni) baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya ufisadi na utoaji zabuni ya barabara yenye thamani ya zaidi ya Sh11 bilioni (Ksh588 milioni).
Akisoma hukumu hiyo leo Alhamisi Februari 13,2025, Hakimu Mkuu wa mahakama ya jimbo hilo, Thomas Nzioki amesema mbali na Waititu, mahakama hiyo pia imemhukumu mke wake, Susan Wangari, kifungo cha mwaka mmoja jela ama kulipa faini ya zaidi ya Sh10 milioni (Ksh500,000).
Waititu na mkewe, Susan Wangari, walitiwa hatiani jana Jumatano Februari 12, 2025, na hukumu yao kusomwa leo Februari 13, 2025.
Walikuwa wanakabiliwa na makosa ya mgongano wa maslahi na kujipatia mali yenye utata, baada ya kupokea mamilioni ya fedha kwa njia ya rushwa kupitia zabuni ya ujenzi wa barabara Jimbo la Kiambu nchini humo.