Matumizi Ya Kondomu Yamepungua Tanzania

Matumizi Ya Kondomu Yamepungua Tanzania

Serikali imesema matumizi ya kondomu wakati wa tendo la ngono nchini yamepungua kwa kiasi kikubwa, hali inayoongeza hofu ya kuongezeka kwa maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi (VVU).

Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Ziada Sellah amesema hayo jini Dodoma leo Alhamisi Februari 13, 2025 wakati wa uzinduzi wa Siku ya Kondomu Kimataifa ambayo nchini Tanzania imefanyika kwa mara ya kwanza.

Ziada amesema utafiti inaonekana matumizi salama na sahihi ya kondomu yamepungua kwa kiasi kikubwa nchini.

“Tunapoacha kutumia kondomu tunajiweka kwenye mazingira magumu ya kuwa na ongezeko la mimba zisizotarajiwa na magonjwa mengine ya zinaa,’ amesema Ziada.

Hata hivyo, taarifa za Wizara ya Afya zinaonyesha maambukizi ya VVU yamepungua kwa asilimia 2.6.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button