Jay-Z Nafamilia Yake Waonekana Hadharani.

Jay-Z Nafamilia Yake Waonekana Hadharani.

Beyoncé, Jay-Z, na binti yao wa miaka 12,
Blue lvy Carter, walijitokeza hadharani kwenye tamasha la filamu ‘Mufasa: The Lion King’ Jumatatu Desemba 9, siku moja baada ya Jay-Z kukanusha madai ya ubakaji dhidi
yake.

Beyoncé, mwenye umri wa miaka 43, amerudia nafasi yake kama Nala kwenye filamu hiyo mpya ya Disney, ambayo ni sehemu ya ‘The Lion King’ ya 2019, ikitarajiwa kuonyeshwa kuanzia Desemba 20. Blue Ivy naye amepewa nafasi ya Kiara, simba mdogo wa kike.

Familia hiyo ilipiga picha kwenye zulia jekundu kwenye ukumbi wa Dolby Theatre, Los Angeles. Jay-Z, mwenye miaka 55, anatuhumiwa kumbaka msichana wa miaka 13 miaka 24 iliyopita, madai yaliyotolewa kwenye kesi ya madai mwezi Oktoba na mwanamke anayejulikana kama Jane Doe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button