Kenyatta, Raila Wahudhuria Misa ya Waliouawa Kwenye Maandamano Kenya.
Rais Mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ni miongoni wa vigogo wa Azimio, ambao wamefika katika Kituo cha SKM cha jini Nairobi Kenya, kuhudhuria misa ya kuwaombea waliofariki wakati wa maandamano dhidi ya Serikali nchini humo.
Maandamano hayo yaliyoitishwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga, yalikuwa na lengo la kupinga kupanda kwa gharama za maisha nchini humo, lakini pia kuulalamikia uchaguzi uliopita, ambao ulimuingiza madarakani Rais William Ruto.
Pamoja na Kenyatta, vigogo wengine wa Azimio ambao wamehudhuria misa hiyo ni pamoja na kiongozi wa Azimio Raila Odinga, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka na Kiongozi wa kambi ya wachache bungeni, Opiyo Wandayi.
Hapo awali misa hiyo ilipangwa kufanyika katika kituo cha De Paul kilichopo Karen, jijini Nairobi; lakini taarifa za ndani zinasema kuwa
ukumbi huo ulibadilishwa baada ya polisi kudaiwa kukionya kituo hicho, kutoandaa maombi hayo.