Kisa Azam Fc Diarra, Aucho waitwa Avic Haraka na Gamondi
“Nimefurahishwa na mabadiliko ya ratiba kwani nilikuwa naumiza kichwa namna ya kupata mechi ya kirafiki ili kuwajenga kimwili na kiushindani wachezaji wangu ambao wamekaa nje ya uwanja kwa muda bila mechi (Ya ushindani)”
“Wachezaji wote wameshaingia kambini isipokuwa wale ambao waliitwa kwenye timu za taifa. Ni wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza wameitwa kwenye timu zao za taifa hilo haliondoi mimi kuendelea kuwaandaa wachezaji waliopo na wao pia wana mchango kwenye timu”
“Yanga haimtegemei mchezaji mmoja, wote wanategemeana hivyo kurudi kwa wachezaji ni mwanzo mzuri wa kuwaandaa tayari kwa ajili ya mchezo ulio mbele yetu, hautakuwa Mchezo rahisi tunakutana na timu ambayo haijapoteza Mchezo hata mmoja (Azam FC), hicho ni kipimo sahihi cha mechi za ushindani,”
Miguel Gamondi”Djigui Diarra, Stephane Aziz Ki na Khalid Aucho wanacheza mechi zao za mwisho za kirafiki, wakitumikia timu zao za taifa 18 October .. nimewaambia warudi siku inayofuata (19 October) ili kujiandaa na Mchezo ulio mbele yetu”