Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa, ameshiriki kufuatilia mashindano ya Knock Out ya Mama
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa, ameshiriki kufuatilia mashindano ya Knock Out ya Mama yanayoendelea katika viwanja vya Posta Kijitonyama, jijini Dar es Salaam Oktoba 10, 2025.
Mashindano hayo yanahusisha mabondia mahiri wa Tanzania wanaopambana na mabondia kutoka nchi mbalimbali ikiwemo India, Pakistan, Uganda Malawi na nyinginezo ikiwa ni sehemu ya kukuza na kuendeleza mchezo wa ngumi nchini.







