Mtanzania Novatus Dismas Miroshi amecheza mechi yake ya kwanza ya UEFA Champions League

Mtanzania Novatus Dismas Miroshi  “Novatus40”  amecheza mechi yake ya kwanza ya UEFA Champions League akiwa na Timu yake ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine ambayo imecheza na FC Porto ya Ureno.

Kwa mechi hiyo waliyofungwa 3-1 na ambayo Novatus alicheza kwa dakika zote 90 kumemfanya Novatus kuwa Mchezaji wa tatu katika historia ya Tanzania kuwahi kucheza michuano ya UEFA Champions.

Watanzania wengine waliowahi kucheza michuano hii ni Mbwana Samatta akiwa kama Mtanzania wa pili na Kassim Manara ambaye ndio Mtanzania wa kwanza kucheza michuano hii

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button