Ulenga Akemea Rushwa na Ubabaishaji Temesa

Ulenga Akemea Rushwa na Ubabaishaji Temesa

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amekemea
vitendo vya ubabaishaji na rushwa miongoni mwa Watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umemne Tanzania (TEMESA) akisema vinaweza kufuta mazuri yote ambayo
Taasisi hiyo imeyafanya na inaendelea kuyafanya.

Akiongea na Menejimenti ya TEMESA na Mameneja wa Mikoa Jijini Dodoma, Waziri Ulega ameeleza Serikali imedhamiria kuifanya TEMESA kuwa Taasisi namba moja
na kimbilio la wote katika utengenezaji wa magari ya Serikali na binafsi.

“Tunatakiwa kupiga vita sana vitendo vya ubabaishaji na rushwa, huu ndio ugonjwa unaoharibu Taasisi nyingi na kwakweli tunahitaji kutumia uwezo wetu wote
kupambana na jambo hili”

Huo ulikuwa ni mkutano wa kwanza baina ya Waziri Ulega na Viongozi wa TEMESA tangu ateuliwe kuwa  Waziri wa  Wizara hiyo mwezi huu

“Hongereni kwa kuanzisha mkakati mpya wa kufanya kazi utakaowawezesha
kujiendesha kibiashara kwa kushirikiana na Sekta binafsi pale inapobidi ili kuihudumia Jamii kikamilifu, sisi TEMESA lazima tuwaoneshe Watu ukinilipa nitakufanyia
kazi kwa wakati”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button