Waajiri Wataka Roboti Kuliko Wasomi wa Gen-Z
Waajiri Wataka Roboti Kuliko Wasomi wa Gen-Z
Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Hult
International Business School umebaini kuwa takribani 37% ya waajiri wangependelea kuajiri roboti za Al badala
ya wasomi wapya wa kizazi cha Gen Z.
Sababu kuu zinazotajwa na waajiri ni wasiwasi juu ya maadili ya kazi, uzoefu na ujuzi wa wahitimu wapya.
Alinatoa utendaji thabiti, kasi, na uwezo wa kurahisisha kazi, jambo linalosababisha mashirika mengi kuangazia teknolojia badala ya wafanyakazi wa binadamu.
Hata hivyo, hii inaleta mjadala mpana kuhusu mustakabali wa ajira na umuhimu wa wahitimu kujiimarisha katika ujuzi wa kiteknolojia ili kuendana na mabadiliko ya soko la ajira.