Ajiua Kwa Stress za Ugumu wa Maisha Morogoro
Ajiua Kwa Stress za Ugumu wa Maisha Morogoro
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limesema
Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Nungu Nassoro (25), Mfanyabiashara na Mkazi wa Kata ya Lukobe, Wilaya na Mkoa wa Morogoro amekutwa akiwa amejiua kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani
kwenye mti wa mwembe uliopo kwenye makazi yake huku Polisi wakisema chanzo cha kujiondoa uhai wake ni msongo wa mawazo unaotokana na ugumu wa maisha.
Taarifa iliyotolewa leo March 02,20:25 na Kamanda wa Polisi Morogoro imesema “Tukio hili limebainika mapema jana March 01, 2025 katika Mtaa na Kata ya Lukobe,
Manispaa ya Morogoro”
“Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo kujiondoa uhai ni msongo wa mawazo unaotokana na ugumu wa maisha, maiti imekabidhiwa kwa Ndugu wa marehemu
baada ya kukamilisha uchunguzi wa
maiti hiyo”