Zuchu 2025: Mwaka wa Kuandika Historia

Zuchu 2025: Mwaka wa Kuandika Historia

Mwaka 2025 ulikuwa mwaka wa kipekee kwa Zuchu, msanii wa kike aliyeendelea kuthibitisha nafasi yake kama nguvu kubwa ya muziki Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Kwenye kipindi hiki, Zuchu aliweka rekodi mpya kwa kuwa msanii wa kwanza wa kike Afrika Mashariki kufikisha views bilioni 1 You Tube, hatua iliyothibitisha ukubwa wa ushawishi wake kwenye jukwaa hilo la viedeo.

Kimataifa, Zuchu aliendelea kupenya kwa kasi kupitia wimbo wake “Amanda” na remix yake aliyofanya na malkia wa Dancehall Spice, ambao uliingia kwenye chati za Billboard za Marekani (Reggae) huku ukikusanya zaidi ya posti milioni 1.3 Tik Tok. Mwaka huu, @officialzuchu aliandika historia kwa ku-headline Yanga Day pamoja na ku-headline CAF Halftime Show 2025 nchini Kenya.

Kwa upande wa tuzo na heshima, Zuchu alitwaa Best Female Global Artist kwenye African Golden Awards, akiwapiku wasanii wakubwa wa Afrika. Pia aliendelea kuonekana kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, kusaini mikataba ya ubalozi, na kutambuliwa kama msanii wa kike wa Tanzania aliyesikilizwa zaidi mwaka 2025 kwenye majukwaa ya Spotify, Boomplay, YouTube na Audiomack.

Kwa ujumla, 2025 ilikuwa mwaka wa uthibitisho, Zuchu hakuvunja rekodi peke yake, bali aliweka viwango vipya vya mafanikio kwa wasanii wa kike kutoka Afrika Mashariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button