Ali Kamwe : Safari ya kwenda kigali Rwanda yapamba Moto

 

Timu inatarajia kuondoka tarehe 14.09.2023 (Alhamisi) kuelekea Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kwanza raundi ya pili #CAFCL dhidi ya Al-Merrikh SC.

Najua watanzania wengi wanayo kiu ya kwenda kushuhudia mchezo wetu dhidi ya Al-Merrikh. Klabu imeaanda mpango wa kusafiri na mashabiki kutoka hapa Dar es Salaam kwenda Kigali, Rwanda. Wachezaji na benchi la ufundi watasafiri kwa njia ya anga, mashabiki na Viongozi watasafiri kwa njia ya basi”

Tutakuwa na mabasi rasmi ambao Uongozi wa Young Africans umeendaa. Kila ambaye anahitaji kwenda atahitajika kutoa kiasi cha tsh. 150,000 ikiwa ni nauli ya kwenda na kurudi. Utaratibu wa kula kunywa na kulala kila mtu atajitegemea mwenyewe. Hata hivyo kila mtu atapaswa kuwa na hati ya kusafiria.

Tumepokea jumbe mbalimbali kutoka Rwanda wakitusubiria kwa hamu kubwa. Rwanda nzima inayo kiu kubwa ya kutupokea. Misafara yote itaondoka siku moja. Kwa wale wanaotumia basi wataondoka hapa tarehe 14.09.2023 saa 11 alfajiri, na kwenda kulala Kahama kabla ya kuelekea Rwanda. Kurudi itakuwa tarehe 17 au tunaweza kuongeza siku”

“Tunatarajia kuwa na mchezo wa kirafiki wikiendi hii. Tutatangaza tunacheza na timu gani. Hata hivyo tunatoa fursa kwa timu yoyote inaweza kuomba mchezo wa kirafiki na sisi tutacheza popote pale”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button