Azam Fc kukipiga na Gor Mahia jijini Nairobi

Azam FC inatarajia kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Kenya (FKF-PL), Gor Mahia, jijini Nairobi, Novemba 19.

 Azam inakwenda kucheza mechi hiyo ikiwa ni moja ya maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Novemba 24, kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam. Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zacharia ‘Zaka Zakazi’

 Amesema 🗣.” Unajua timu zote ambazo tungetaka kucheza nazo hapa ni zilezile tunazokutana nazo kwenye ligi, hivyo kusingekuwepo na tofauti yoyote ndiyo maana tumeona tucheze na Gor Mahia mechi ambayo itakuwa na tofauti kubwa.”

“Timu itaondoka Novemba 18, siku itakayofuata tutacheza mechi na baada ya mechi tutarudi (nchini) kuendelea na maandalizi ya mwisho ya kucheza na Mtibwa Suga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button