Singida fountain imefungiwa kusajili

Klabu ya Singida FG imefungiwa kusajili usajili wa kimataifa na usajili wa ndani kutokana kutomlipa aliekuwa mchezaji wao Nicholas Gyan raia wa Ghana

Singida FG imefungiwa na Shirikisho la mpira wa miguu duniani “FIFA” kufanya usajili wa kimataifa kutokana na kushindwa kesi ya madai iliyofunguliwa na mchezaji huyo baada ya kushinda kesi yake inayohusu malimbikizo ya mishahara pamoja na hela za ada ya usajili.

FIFA imeiamulu Singida FG kumlipa stahiki zote Nicholas Gyan ndani ya siku 45 tangu hukumu iliyotoka, vinginevyo suala hilo litapelekwa kamati ya nidhamu ili kuchukuliwa hatua zaidi za kinidhamu.

wakati FIFA ikiifungua Singida FG Fc kufanya usàjili wa kimataifa pia Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania “TFF” limeifungia timu hiyo ya kufanya usajili wa ndani mpaka itakapomlipa mchezaji huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button