Hii ni wiki yetu, kama kuna mtu kinamkera aende hata Tanga

Viingilio tumepanga kwa kuangalia hali za watu wetu.
Platinum – Tsh. 200,000
VIP B- Tsh. 40,000
VIP C – Tsh. 30,000
Machungwa – Tsh. 10,000
Mzunguko – Tsh. 7,000.

Hatutakuwa na VIP A sababu jukwaa limechukuliwa na FIFA na CAF.”

“Tiketi tayari zimeanza kuuzwa vituoni.”

“Tutazunguka Dar nzima kufanya hamasa. Tarehe 14 ndio tutazindua wiki ya Kispika (Wiki ya Hamasa), tutazindulia Coco Beach. Kutakuwa na matukio mbalimbali kama mechi za mashabiki na pia kutakuwa na watu wa kuuza tiketi, watu wa NMB na CRDB kwa ajili ya watu kupata namba za mashabiki lakini pia jezi zitauzwa pale.”

“Hii ni wiki yetu, kama kuna mtu kinamkera aende hata Tanga. Hiyo tarehe 14 tutaanzia maandamano kutokea makao makuu ya klabu kwenda Coco Beach. Tunatarajia kufika Coco majira ya saa 4 asubuhi.”

“Jumapili itakuwa mapumziko kidogo. Jumatatu tutakuwa na Paint the City, hiyo siku ni kubandika vipeperushi kila sehemu. Kwenye mstimu, kwenye geti, kwenye magari. Hakuna mtu ambaye hatajua kama Simba inacheza tarehe 20.”- Ahmed Ally. #AFL #WenyeNchi #NguvuMoja

Mechi itachezwa saa 12:00 jioni kwenye Uwanja wa Mkapa ambao na Simba imechangia ukarabati wake hivyo wajue wakicheza kwenye uwanja ule wanacheza sehemu ambayo Simba imechangia ukarabati.”

“Watu wa African Football League wamefurahia ilivyokuwa programu ya Simba Day hivyo kwa kiasi kikubwa inafanana na kuna maboresho wamefanya.”

“Kesho Alhamisi kikosi kitaingia kambini baada ya kumnyoa Singida Fountain Gate. Kuhusu wachezaji walioitwa timu za taifa tunaendelea na mazungumzo na mashirikisho ili wachezaji waliotwa wawahi kurudi ili tujiandae kwa ubora zaidi.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button