Je tutampa tena mburudishaji kama Neymar ?

 

✍️ Miguu yenye uwezo mkubwa sana wa kucheza soka la kuvutia, akili kubwa ya kumtesa mpinzani kwa soka lenye mvuto na mwonekano wa kistaa tangu akiwa kijana mdogo. Ni kama alizaliwa ili aje kuwa staa mkubwa wa soka duniani.

✍️ Amewahi kuwepo kwenye orodha ya wachezaji kumi bora duniani kwa mujibu wa tuzo za Ballon d’or kabla hata hajagusa ardhi ya Ulaya. Alishaingia mioyoni mwa wapenda soka wakati akiwa mdogo sana.

✍️ Nilitamani sana carrier yake isiishe hivihivi bila hata tuzo moja kubwa kama ya Ballon d’or au ile ya FIFA. Hii ni tamaa yangu ambayo ni kama Neymar ameamua kuiua rasmi baada ya kwenda Saudi Arabia. Siioni tena nafasi hiyo.

✍️ Neymar ni kati ya wale wachezaji ambao kwao mchezo wa mpira wa miguu ni zaidi ya kupata matokeo ya kushinda. Ni zaidi ya kupata alama tatu kiwanjani. Anatuaminisha kuwa soka ni burudani na mvuto kwa watu kuangalia.

Kutamba kwenye kipindi cha Messi na Ronaldo pengine imekuwa gundu kwake kwenye majukwaa ya tuzo kubwa.
Je, tutampata tena mburudishaji kama Neymar Jr??

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button