Jemedari Sc iheshimiwe na Robertinho aheshimiwe aachwe afanye kazi yake

SIMBA SC IHESHIMIWE FT 1-1 (Agg 3-3), ROBERTINHO AHESHIMIWE AACHWE AFANYE KAZI YAKE.

 

Kanuni ya bao la ugenini imeiondoa Simba SC kutoka kwenye mashindano ya African Football League (AFL). Baada ya sare ya nyumbani ya 2-2 Leo imetoka sare nyingine ya ugenini ya 1-1 pale Cairo Misri dhidi ya Ahly. Sio kila timu inaweza kuidindia Ahly namna hii hasa ukanda huu wa CECAFA, Ahly ndio klabu ya Karne, ndiyo klabu ya kihistoria Afrika, klabu namba 1 kwa ubora Afrika kwa sasa, ndiyo Mabingwa watetezi wa CAF CL wakishinda mara 11 ambayo ni rekodi

 

Haikuwa rahisi kwenye mechi zote 2 Simba wameonyesha kwanini wao walistahili kuwapo AFL kutoka CECAFA na sio timu nyingine, wameonyesha kwanini wao ni klabu bora Tanzania na CECAFA yote kwa miaka 5 mfululizo.

 

There are always next time boys, you fought a lot but wasn’t your luck, heads up

 BIN KAZUMARI (The voice of the voiceless)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button