Mtoto wa Diddy naye ashitakiwa kwa unyanyasahi wa kingono
Mtoto wa nyoka ni nyoka, kijana wa Diddy naye huwenda akajikuta anaingia matopeni kwani mwanamke mmoja ambaye hakuanika jina lake, amepanga kumfungulia mashtaka ya unyanyasaji wa kingono. Mwanasheria Tyrone Blackburn, ambaye anawawakilisha wanawake kadhaa ambao wanamtuhumu Diddy kwa vitendo hivyo amesema kesi hiyo ipo kwenye hatua za mwisho kufunguliwa.






