Neymar atarajia kupata mtoto
Mchezaji wa Klabu ya PSG, Neymar na mpenzi wake Bruna Biancardiare wanatarajia kupata mtoto.Nyota huyo wa Brazil ametangaza matarajio yake ya kupata mtoto mwingine.
Mtoto huyo atakuwa wa pili kwa Neymar baada ya yule wa kwanza mwenye umri wa miaka 11 anayejulikana kwa jina la Davi Lucca.
Haijafahamika kama wawili hao wanatarajia kupata mtoto wa kiume ama wa kike.





