Sehemu ya kwanza: Kumuhusu SIMBAMANGU (Caracal).
SEHEMU YA 1.
UTANGULIZI
Ushawahi kusikia kuhusu paka mdogo wa porini aitwaye simbamangu ama Caracal? Unaweza kumuangalia vizuri kwenye post iliyopita akiwa kasimama ama kwenye post hii pia. Nitakuletea na picha zingine kwenye makala hii hii.
PAKA WA PORINI.
Hapa ngoja tuwekane sawa kwanza kwa uchache na kwa lugha rahisi kidogo ili watu waelewe. Watu wengi wamekuwa wakichanganya mambo kila nikisema simba ni paka, chui ni paka, duma ni paka, mara mondo ni paka, huyu nae wa leo simbamangu ni paka. Kipi ni kipi sasa? 😁👌
Uhalisia ni kuwa tuna paka wengi sana karibia spishi 41 hivi duniani akiwemo paka tunayemfuga majumbani. Wanagawanyika kwenye makundi kulingana na saizi ya maumbo yao ambapo tuna paka wakubwa wa porini na paka wadogo wa porini. Unaweza kuwapata sehemu tofauti tofauti za ma bara hapa duniani.
PAKA WAKUBWA WA PORINI.
Paka wakubwa kwa hapa kwetu tanzania ndo hao kina simba, chui na duma, pia kuna wengine ambao wapo ma bara mengine kama tiger, jaguar na wengineo.
PAKA WADOGO WA PORINI.
Hawa paka wadogo ndo wapo kina mondo (serval cat), huyu wa leo simbamangu (Caracal) na wengineo wengi tu kwenye kundi lao hilo.
Hawa wote paka wakubwa na wadogo wanakuwa wanatofautiana kwa vitu vichache vichache kulingana na mahali wanapopatikana, chakula, mazingira, na mengine mengi kama hayo.
Hapo nadhani kidogo umeshaanza kupata mwanga sasa wa nini namaanisha nikisema paka wakubwa wa porini ama paka wadogo wa porini sio? 🤷♀️
Sasa tuendelee na makala yetu ya leo kumhusu huyu paka aitwaye simbamangu (Caracal) 😋👇
SIMBAMANGU (Caracal) NI NANI SASA?
Huyu ni jamii ya paka wadogo ambaye ndo mkubwa zaidi na mwenye nguvu kuliko wengine kwenye hili kundi la paka wadogo.
ASILI YA JINA LAKE.
Jina lake lina asili ya uturuki “karakulkak” likimaanisha “sikio jeusi”. Ni moja kati ya jamii chache za paka wasio na madoa doa ama mistari kwenye miili yao. Ni paka waliojaaliwa usikivu sana, moja ya silaha yao kubwa sana kwenye uwindaji, hasa kunasa mawimbi ya sauti ndogo zaidi za wanyama anaowawinda.
Makala hii imedhaminiwa @winn_licious