Travis Amaliza Kesi 100 Janga la Astroworld
Travis Amaliza Kesi 100 Janga la Astroworld

Travis Na Kampuni Ya Live Nation Wameripotiwa Kumaliza Karibu Kesi 100 Za Majeruhi Na Walioathirika Katika Janga Lilitokea Kwenye Tamasha Lake La Astroworld Novemba 2021.
Pia Inadaiwa Bado Kesi Zingine Zaidi Ya 100 Zinazomkabili Kutokana Na Janga Hilo.
Usiku wa Novemba 5, 2021 hautapotea kichwani mwa Travis Scott baada ya kushuhudia watu 10 wakipoteza maisha, 25 wakilazwa na 300 wakitibiwa kwa kupata
majeraha kufuatia msongamano wa mashabiki uliopelekea watu kuangushana (crowd crush).



Kumbuka Pia Travis Aliandaa Tamasha hilo Ili mapato Yatakayopatikana Yaende kwenye mfuko wa taasisi Yake itwayo Cactus Jack Foundation kwa ajili ya kusaidia vijana wadogo kupata elimu.
Baadhi ya wasani Wengine ambao Walitumbuiza kwenye tamasha hilo ni 21 Savage, Lil Baby, SZA, Bad Bunny, Roddy Ricch na wengine kibao.





