Viongozi Yanga washituka Mtego waliowekewa na Medeama
Yanga jana ilipotua Accra, Ghana mabosi wao walishtuka mchezo huo kupelekwa Jiji la Kumasi na kama safari hiyo wangetumia Basi wachezaji wao watachoka. .
Wakakodisha ndege maalum ambayo ilibeba timu hiyo kutoka Accra kwenda Kumasi.
Kwa ndege hiyo, Yanga ilitumia muda wa dakika 35-60 pekee kufika Kumasi hesabu ambazo ziliwapunguzia uchovu ambapo kama wangetumia Barabara wangekaa masaa yasiyopungua manne kusafiri kilomita 202. .
Yanga imechukua hoteli ya kisasa ya Ridge Condos yenye hadhi ya nyota 4.4 ambayo ndio hoteli ambayo inatumiwa na timu mbalimbali kubwa zinazofika jijini hapo.