Augustine Okrah Ajiunga na Yanga Kutangazwa Zanzibar

Kiungo mshambuliaji aliyewahi kucheza Simba SC Augustine OKRAH amekamilisha usajili wake wa kujiunga na Yanga na amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania.

Okrah ambaye tayari Yuko Zanzibar atatambulishwa siku ya jumapili ikiwa ni usajili wa kigeni baada ya kocha kupitisha usajili wake akija kuchukua nafasi ya Jesus Ducapel Moloko.

Okrah ataanza kuitumikia Yanga katika michuano ya Mapinduzi ambapo Yanga wataanza kutupa karata yao siku ya jumapili saa 2:15 usiku. Okrah amekuwa kwenye kiwango bora baada ya kuachana na Simba na kujiunga na klabu yake ya zamani Bechem United alipofunga magoli tisa mpaka anajiunga na Yanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button