Dhoruba Nor’eaester Yaipiga Marekani Mafuriko na Upepo Mkali Vyatikisa
Dhoruba Nor'eaester Yaipiga Marekani Mafuriko na Upepo Mkali Vyatikisa
Dhoruba kali ya Nor’easter imeendelea kuathiri maeneo ya Pwani ya Mashariki ya Marekani, ikileta upepo mkali, mvua kubwa na mafuriko ya ghafla, huku hali ya hewa ikitarajiwa kuendelea kuwa mbaya hadi kuelekea jioni.
Mafuriko ya pwani yanatarajiwa kuwa makubwa zaidi katika kipindi cha saa mbili kabla na baada ya maji kujaa, huku Atlantic City, New Jersey, ikitarajiwa kufikia kiwango chake cha juu zaidi cha maji majira ya saa 8:00 usiku kwa saa za Marekani (ET).
Dhoruba hiyo imeongeza hatari kwa wakazi wa maeneo ya chini na ya karibu na bahari, huku mvua kubwa ikisababisha maji kujaa kwa kasi katika baadhi ya maeneo. Mamlaka zinaendelea kufuatilia hali hiyo kwa karibu, huku wakazi wakitakiwa kuwa waangalifu kutokana na hatari ya mafuriko ya ghafla, upepo mkali na kuongezeka kwa kina cha maji katika maeneo ya pwani.






