TRA wabaini Taarifa Zisizo Sahihi kwenye G Wagon ya Ommy Dimpoz

TRA wabaini Taarifa Zisizo Sahihi kwenye G Wagon ya Ommy Dimpoz

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema imebaini tofauti katika taarifa za forodha za gari aina ya Mercedes-Benz G-Wagon linalohusishwa na msanii wa Bongo Fleva na mfanyabiashara, Omary Nyembo maarufu Ommy Dimpoz, baada ya uchunguzi wa kitaalamu kubaini kuwa gari hilo ni la thamani kubwa zaidi kuliko lilivyoelezwa wakati wa uingizaji nchini.

TRA imesema gari hilo lililoonekana kwenye video iliyosambaa mitandaoni, likionyesha maofisa wa mamlaka hiyo wakilikagua. Huku kukiwa na mabishano atika eneo la tukio, lilikuwa sehemu ya operesheni inayoendelea ya ukaguzi wa magari kwa lengo la kubaini uwepo wa ukwepaji kodi.

Kwa mujibu wa taarifa ya TRA, operesheni hiyo ilianza Septemba 26, 2026, na katika ukaguzi huo maofisa walilikuta gari hilo likiwa limeegeshwa katika Palm Beach Casino jijini Dar es Salaam bila namba za usajili. Baada ya hapo, TRA ilianza mchakato wa kubaini utambulisho wa gari hilo na historia yake katika mfumo wa forodha.

Mamlaka hiyo imesema uchunguzi wa kitaalamu uliwezesha kubaini namba maalumu ya utambulisho wa gari (VIN) kuwa WDB4632762X322756. Ambayo baadaye ilihakikiwa katika Mfumo wa Forodha wa Tanzania (TANCIS).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button