Mafuriko Makubwa Bangkok zaidi ya Kaya 52000 Zahadhirika

Mafuriko Makubwa Bangkok zaidi ya Kaya 52000 za Hadhirika

Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa siku kadhaa katika mji mkuu wa Thailand, Bangkok, yamefurika nyumba na barabara, huku takribani kaya 52,000 zikiathirika na karibu watu 4,900 wakihamishwa na kupelekwa katika maeneo ya hifadhi.

Mamlaka ya Jiji la Bangkok (BMA) imesema viwango vya maji katika mtandao wa mifereji ya jiji vilibaki kuwa juu hadi Jumapili asubuhi, huku juhudi zikiendelea kuharakisha uondoaji wa maji. Mamlaka pia imetahadharisha kuwa mvua zaidi zinatarajiwa kunyesha Bangkok na maeneo ya jirani siku ya Jumapili, ingawa mvua hizo zinatarajiwa kupungua kuanzia Jumatatu.

Mamlaka zilitangaza hali ya maafa ya mafuriko katika jiji lote la Bangkok Jumamosi, baada ya mvua kubwa kunyesha kwa karibu saa 48 mfululizo. Kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa, baadhi ya maeneo ya Bangkok yalipokea zaidi ya milimita 330 za mvua, sawa na takribani inchi 13, katika kipindi cha kuanzia Alhamisi hadi Jumapili.

Wanasayansi wanaonya kuwa ongezeko la joto duniani linalochangiwa na uzalishaji wa hewa chafu kutoka kwenye matumizi ya nishati za kisukuku linaweza kuongeza ukubwa na mara kwa mara kwa matukio ya hali mbaya ya hewa, ikiwemo mvua kubwa na mafuriko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button