Shirikisho la soka la Uganda limesitisha mkataba Milutin Sredojević

RASMI: Shirikisho la soka la Uganda limesitisha mkataba wa aliyekuwa kocha wa timu ya Taifa ya Uganda (The Uganda Cranes), Milutin Sredojević kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Micho amevunjiwa mkataba baada ya kushindwa kuisaidia timu ya Taifa ya Uganda kufuzu Afcon2023.

Uganda walikuwa kundi moja na timu ya taifa ya Tanzania, katika mechi za mwisho, Uganda walikuwa wanahitaji kushinda huku wakiiombea Stars ambayo ilikuwa inahitaji sare katika mechi dhidi ya Algeria ipoteze, baada ya matokeo ya mwisho Stars walitoka sare tasa na kufuzu Afcon huku Uganda wakishinda goli 2-0 lakini ushindi huo haukuwasaidia kufuzu.

Baada ya Stars kupata sare ugenini, aliyekuwa kocha Uganda Micho alinukuliwa na chombo kimoja cha habari akisema

🎙️”ameshangazwa sana Stars kupata sare ugenini tena dhidi ya timu bora kama Algeria”.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button