Tajiri Bakhresa atenga zaidi ya milioni 500 kuiuwa Yanga SC kwa mkapa leo

BAKHRESA ATENGA ZAIDI YA MILIONI 500 KUIUA YANGA SC KWA MKAPA LEO.

Azam FC leo Jumatatu itakuwa mgeni wa Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu mzunguko wa sita mechi itakayochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa na tayari mastaa wa matajiri hao wa Chamazi wametengewa kitita cha fedha mezani kama watashinda mechi hiyo.

Taarifa kutoka ndani ya Chanzo chetu kilibaini kuwa Tajiri wa kikosi hicho Yusuph Bakhresa ametenga zaidi ya Tsh 500 milioni kwa timu hiyo kama itaifunga Yanga.

Miongoni mwa mechi muhimu kwetu ni pamoja na hii ya Yanga. Tunataka kushinda ili kuendelea kukaa juu kwenye msimamo.”

“Na nikuambie, kila mtu ndani ya timu anaitaka mechi hii, tajiri tayari ameahidi zaidi ya Sh500 milioni kwa wachezaji na benchi la ufundi kama tutashinda, unaona ni mechi rahisi?

Amesema kiongozi huyo.

Hata hivyo, Azam imekuwa ikikutana na ugumu dhidi ya Yanga katika mechi tano Wanachamazi hao wameambulia sare moja tu kufungwa nne.

Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na alama 13 baada ya mechi tano, huku Yanga ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 12 na nafasi ya kwanza ipo Simba yenye alama 15 baada ya michezo mitano.

Ligi Kuu Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa ambapo macho na masikio ya mashabiki wa soka nchini yataelekezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa wakati Yanga itakapokuwa inaikaribisha matajiri wa jiji la Dar es Salaam, Azam FC.

Mchezo huu utakaopigwa saa 12:30 usiku unatazamiwa kuleta upekee kwani timu yoyote itakayoshinda itaongoza ligi ambapo Yanga itafikisha pointi 15 sambamba na Simba ingawa zitatofautiana zaidi kwenye michezo na mabao ya kufunga na kufungwa.

Kwa upande wa Azam ambayo haijapoteza mchezo wowote kati ya mitano iliyocheza, endapo itashinda pia itafikisha pointi 16 na kukwea kileleni jambo ambalo linaongeza msisimko na ushindani mkali kwa miamba hii wakati itakapokuwa inapambana leo.

Mechi hii ni kisasi zaidi kwa Azam kwani mara ya mwisho ilipokutana na Yanga ilikuwa ni Agosti 9, mwaka huu katika Kombe la Ngao ya Jamii hatua ya nusu fainali na kupoteza mabao 2-0, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button