Moses Matovu afariki akidaiwa kushambuliwa na Majambazi

Moses Matovu afariki akidaiwa kushambuliwa na Majambazi

Mwanamuziki mkongwe wa Jazz na Rhumba kutoka Uganda, Moses Matovu, ambaye alikuwa mwanzilishi wa bendi maarufu ya Afrigo Band, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 77 baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana katika eneo la Kibuli, jijini Kampala. Kwa mujibu wa taarifa za Polisi nchini Uganda, Matovu alishambuliwa na watu hao katika eneo la Kibuli Market Zone B. Kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya Kibuli kwa ajili ya matibabu, ambako baadaye alifariki dunia.

Kifo chake kimekuja wakati ambapo muziki wa Uganda unaendelea kuomboleza kuondokewa na mmoja wa wanamuziki waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya jazz, rhumba na muziki wa dansi nchini humo. Tukio la kushambuliwa na uchunguzi wa polisi Taarifa za vyombo vya habari vya Uganda zinaeleza kuwa Matovu alishambuliwa katika eneo la Kibuli Market Zone B, Makindye Division, Kampala, asubuhi ya Alhamisi, Septemba 24, 2026.

Msemaji wa Polisi wa Kampala Metropolitan, Rachael Kawala, alisema Kituo cha Polisi cha Kabalagala kilifungua jalada la kesi ya mauaji yanayoshukiwa kuhusisha mwanamuziki huyo. Kwa mujibu wa polisi, kikosi cha uchunguzi kilitumwa katika eneo la tukio ili kubaini kilichotokea na kuwatafuta watu waliohusika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button