Russia yarusha makombora Kyiv yauwa watu wawili

Russia yarusha makombora Kyiv yauwa watu wawili

Watu wawili wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa baada ya Russia kushambulia mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, kwa makombora ya balestiki na ndege zisizo na rubani. Shambulizi hilo la leo, Alhamisi, Septemba 24, 2026, lilisababisha vifusi kuanguka katika maeneo kadhaa ya Kyiv, huku mmoja wa waliofariki akiwa katika eneo la maegesho karibu na hospitali ya wazazi na watoto iliyoharibiwa.

Meya wa Kyiv, Vitali Klitschko, amesema watu sita walijeruhiwa, wakiwemo wahudumu watatu wa afya. Wawili kati yao walikuwa katika hali mbaya. Kwa mujibu wa Klitschko, sehemu ya ukuta wa nje wa hospitali hiyo pamoja na kituo cha uchunguzi wa afya kilichokuwa jirani viliharibiwa.

Vifusi vya makombora pia vilianguka katika wilaya kadhaa za Kyiv, ikiwemo Dniprovskyi, ambako nyumba moja iliharibiwa na kulikuwa na taarifa za awali kuhusu uwezekano vwa watu kunaswa chini ya vifusi. Mamlaka ziliwaagiza wakazi kubaki katika maeneo ya kujihifadhi kutokana na hatari va mashambulizi zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button