Pugu Ilipotembeza bakora Tambaza,Kinondoni Muslim

Pugu Ilipotembeza bakora Tambaza Kinondoni Muslim

Kulikuwa na kipindi ambapo jina la Pugu Secondary School lilipotajwa kwenye michezo ya shule Dar es Salaam halikuishia uwanjani. Ushindani mkali ulifanya baadhi ya mechi kuendelea nje ya uwanja, huku Pugu ikijulikana kwa kujibu mashambulizi ilipochokozwa.

Mwanafunzi wa zamani wa Pugu, Leonce Kajilo, anakumbuka mwaka 1989 walipocheza na Tambaza katika mashindano ya Umisseta. Baada ya Pugu kushinda, vurugu zilianza, lakini anasema walikuwa tayari wamejiandaa kukabiliana na hali hiyo.

Anasimulia kuwa kabla ya mechi hiyo, wanafunzi wa Pugu walitengeneza bakora walizokuwa wamezikata maeneo ya karibu na shule, ambazo baadaye zilitumika walipoingia katika mzozo na wenzao wa Tambaza. Kwa mujibu wa Kajilo, Pugu haikuwa shule iliyoanzisha ugomvi, lakini wanafunzi wake waliamini walipaswa kujilinda waliposhambuliwa.

Ushindani huo uliendelea pia dhidi ya Kinondoni Muslim, iliyokuwa na vipaji vikubwa vya soka kipindi hicho. Mbali na soka, Pugu ilijijengea sifa kwa kuwa na wanafunzi walioshiriki michezo kama ndondi, karate na skauti, huku ikijulikana pia kwa kuzalisha wasomi na viongozi mbalimbali nchini.

Katika historia yake, Pugu imewahi kuwa sehemu ya safari ya viongozi wakubwa akiwamo Mwalimu Julius Nyerere aliyefundisha shuleni hapo, pamoja na Rais mstaafu Benjamin Mkapa aliyekuwa mwanafunzi wa shule hiyo. Soma simulizi kamili ya Pugu, Tambaza na Kinondoni Muslim pamoja na historia ya shule hiyo kwenye tovuti ya Mwananchi kesho Jumatano Setemba 23, 2026.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button