Wananchi waliohaama kwa hiari tafadhari El nino wapewe maeneo salama

Wananchi waliohaama kwa hiari tafadhari El nino wapewe maeneo salama

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Gabriel Makalla ameuagiza uongozi wa Wilaya Wilaya ya Monduli na vijiji vya Jangwani na Magadini kufanya utambuzi wa wananchi wao wanaliohama na wanaondelea kuhama katika maeneo yao kwa hiari ili waweze kutambulika na kupata huduma muhimu ikiwemo makazi katika maeneo mengine salama.

Makalla ametoa kauli hiyo leo Septemba 23, 2026 wakati akikagua maeneo hayo hatarishi katika Vijiji vya Magadini na Jangwani, Mto wa Mbu akisema serikali inaendelea na jitihada mbalimbali za kuondoa mafuriko katika eneo hilo. Amesisitiza umuhimu wa wananchi wa Kata ya Mto wa Mbu, kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya mvua za ElniƄo zilizotabiriwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu ikiwa ni pamoja na kuhama katika maeneo hatarishi kulingana na historia ya mafuriko katika eneo hilo.

Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa wananchi hao kuchukua tahadhari, kutokana na historia kata hiyo ya kukumbwa na mafuriko huku akisema ndiyo sababu Serikali imewekeza nguvu kubwa Mto wa Mbu ili kudhibiti athari za mafuriko kutokana na tahadhari ya Elniho iliyotolewa.

Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara, Kamishna msaidizi wa uhifadhi, Eunice Msangi amesema wametoa greda kwa ajili ya uchimbaji wa mfereji huo wa kuzuia mafuriko na ameahidi kuendelea kutoa elimu kuhusu ujio wa mvua hizo za El Nino.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button