Irani ichague Mkataba au Kuangamizwa.
Irani ichague Mkataba au Kuangamizwa
Rais wa Marekani, Donald Trump ameitishia kuiangamiza Iran iwapo haitafikia makubaliano na Marekani, huku akisema nchi hiyo inakabiliwa na uchaguzi kati ya kufanya mkataba wa kumaliza mzozo au kukabiliwa na hatua kali za kijeshi.
Trump alitoa kauli hiyo Jumanne, Septemba 22, 2026, wakati akihutubia Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York, katika kipindi ambacho mzozo kati ya Marekani na Iran unaendelea. “Je, niangamize Jamhuri ya Kiislamu na kufanya hivyo haraka? Je, niwasukume jehanamu bila nafasi ya kuishi wala matumaini ya ukuu wao wa baadaye au vizazi?” Trump alihoji.
Rais huyo amesema Marekani haitaruhusu Iran kupata silaha ya nyuklia, akiongeza kuwa anatarajia Washington na Tehran kufikia makubaliano baada ya uchaguzi wa katikati ya muhula wa Marekani unaotarajiwa kufanyika Novemba 3. Kauli hiyo imekuja wakati mawasiliano ya kidiplomasia kati ya Marekani na Iran yakiendelea licha ya mapigano kati ya pande hizo.





