Pemba Mwanagunzi Auwawa na Kukatwa Kiganja
Pemba Mwanagunzi Auwawa na Kukatwa Kiganja
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba limesema linaendelea na uchunguzi wa tukio la kuuawa kwa Mwanafunzi wa kidato cha kwanza, Raiyan Hemed Amour mwenye umri wa miaka 15, Mkazi wa Kijiji cha Kwale Mpona, Shehia ya Finya, Wilaya ya Wete. Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi iliyotolewa leo Oktoba 5, 2026, mwili wa Mwanafunzi huyo ulikutwa kichakani ukiwa na jeraha la kukatwa kiganja cha mkono wa kulia, kinachodaiwa kukatwa kwa kitu chenye ncha kali.
Polisi imesema Oktoba 2, 2026 saa 12 asubuhi, Mwanafunzi huyo aliondoka nyumbani kuelekea shuleni lakini hakurejea na ilipofika saa 3 usiku siku hiyo, Baba yake alifika Kituo cha Polisi Wete kutoa taarifa ya kupotea kwa Mtoto wake na uchunguzi ukaanza.
Mwili wa marehemu baadaye ulipatikana kichakani na kufanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Wilaya ya Wete, Kinyasini, kabla ya kukabidhiwa kwa Ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi. Jeshi la Polisi limewataka Wananchi kutumia Vituo vya Polisi kuripoti matukio ya kihalifu na kuacha kujichukulia Sheria mkononi, huku likisisitiza kuwa linaendelea na taratibu za kuwatafuta na kuwakamata wahusika ili wafikishwe Mahakamani.





