Wanawake Iran waingia Mafunzo Yakivita
Wanawake Iran waingia Mafunzo Yakivita
Wakati mvutano kati ya Iran, Marekani na Israel ukiendelea, Wanawake nchini Iran wameanza kupata mafunzo ya msingi ya kijeshi na matumizi ya silaha, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuwawezesha kulinda Familia na Jamii zao endapo vita vitatokea.

Katika mafunzo hayo yaliyofanyika Mjini Tehran, Wanawake walionekana wakipokea maelekezo na kushiriki mafunzo ya matumizi ya silaha ikiwa ni sehemu ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na mazingira ya vita. Mafunzo hayo yalifanyika Oktoba 4, 2026, wakati mvutano wa kiusalama kati ya Iran, Marekani na lsrael ukiendelea ambapo kwa mujibu wa Reuters, lengo la mafunzo hayo ni kuwaandaa Wanawake hao kuwa na uwezo wa kuzilinda Familia na Jamii zao endapo vita vitatokea.





