Rubani Afariki Ajalini Siku 16 Baada ya Kuoa
Rubani Afariki Ajalini Siku 16 Baada ya Kuoa
Rubani wa Jeshi la Anga la Nigeria (NAF), Squadron Leader Ahamefule Aham Man-Ugwueje amefariki katika ajali ya ndegeiliyotokea Ondo State, Nigeria ikiwa ni siku 16 tu baada ya kufunga ndoa. Man-Ugwueje, ambaye alikuwa rubani msaidizi (co-pilot) wa ndege aina ya ATR-42 yenye namba NAF 931, alifunga ndoa na Flight Lieutenant Damilola Adekunle Septemba 19, 2026 katika sherehe iliyofanyika Abuja.
Ndege hiyo ilianguka Oktoba 5, 2026 katika eneo la Igbokoda, Ondo State, ikiwa kwenye safari ya kawaida kutoka Benin kuelekea Lagos ambapo Jeshi la Anga la Nigeria limethibitisha kuwa Watu wote 25 waliokuwa ndani ya ndege hiyo, wakiwemo Wahudumu watano na abiria 20, wamefariki.
Jeshi hilo limetangaza kuwa uchunguzi wa kina umeanzishwa ili kubaini mazingira na chanzo cha ajali hiyo, huku likiitaka Jamii kuepuka kusambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa ambapo taarifa rasmi iliyotolewa awali ilitaja waliofarikiwa kuwa ni 32.







