Khamenei: Madini ya urani yatabaki Iran hakuna kutoka nje

Khamenei: Madini ya urani yatabaki Iran hakuna kutoka nje

Kiongozi mkuu wa Iran, Mojtaba Ali Khamenei ameagiza kuwa madini ya urani yaliyorutubishwa yasiruhusiwe kutoka nje ya nchi hiyo, hatua inayoweza kuongeza mvutano katika mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na Marekani.

Kwa mujibu wa Reuters, Iran imeendelea kusisitiza kuwa haitakuwa tayari kusalimisha madini hayo licha ya shinikizo kutoka Marekani kuitaka kusitisha mpango wake wa nyuklia.

Agizo hilo la Khamenei linaelezwa kuwa linaweza kudhoofisha juhudi za kidiplomasia zinazolenga kupatikana kwa suluhu ya mgogoro huo kupitia mazungumzo yanayoendelea.

Awali, Rais wa Marekani, Donald Trump alisema nchi yake haitaruhusu Iran kumiliki madini ya urani yaliyorutubishwa wala kuendelea na mpango wake wa nyuklia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button